
Falsafa na Maadili ya Ualimu Elimu Awali ni kozi iliyoandaliwa mahsusi kwa walimu wanaofundisha madarasa ya awali, la kwanza na la pili inayolenga kumjengea mwalimu kumudu misingi ya kifalsafa, maadili na wajibu wa taaluma ya ualimu. Inamwezesha kutafakari nafasi ya mwalimu katika jamii, kufanya maamuzi yenye misingi ya kimaadili na kuzingatia viwango vya kitaaluma katika ufundishaji na malezi ya watoto.
- Instructor: Novatus Dimoso
- Instructor: Amani Msuya

Saikolojia na Sosholojia ya Ualimu Elimu Awali ni kozi mahsusi iliyoandaliwa kwa walimu wanaofundisha madarasa ya Awali, la kwanza na la pili. inayomwezesha mwalimu kumudu misingi ya kisaikolojia na kijamii inayochangia ukuaji, ujifunzaji na tabia za mtoto. Inalenga kumjengea uwezo wa kumudu kutumia maarifa ya saikolojia na sosholojia kuboresha mahusiano, mazingira ya kujifunzia na ufanisi wa ufundishaji.
- Instructor: Masumbuko Mpoli
- Instructor: Ismail Mussa

Kozi hii inakupa ujuzi wa kuandaa zana bora za uchunguzi na upimaji wa maendeleo ya mtoto, kusimamia tathmini endelevu kupitia michezo na vitendo darasani, na kuchambua maendeleo ya ukuaji wa kila mtoto. Utajifunza jinsi ya kutumia kumbukumbu za maendeleo na tabia za watoto ili kuboresha mbinu za ufundishaji na kutoa msaada wa mapema unaokidhi mahitaji ya kipekee ya kila mtoto wa elimu ya awali.
- Instructor: Admin User

- Instructor: Alfred Mhando

Somo la Mbinu za Ufundishaji na Ujifunzaji Elimu ya Awali na Darasa la I–II humwandaa mwalimu tarajali kupata maarifa, stadi na umahiri wa kutumia mbinu bora za kufundisha stadi za msingi za kuhesabu, kusoma, kuandika, afya, mazingira, sanaa na michezo. Pia, somo linakuza ubunifu katika matumizi ya teknolojia na vifaa vya kufundishia, uchopekaji wa masuala mtambuka, na mbinu za kufundisha madarasa makubwa. Lengo ni kumwezesha mwalimu kuendesha ufundishaji unaozingatia ushirikiano, mawasiliano, udadisi, ubunifu na utatuzi wa changamoto katika Elimu ya Awali na Darasa la I–II.
- Instructor: Asha Chara
- Instructor: Afro Luciana