
Elimu Jumuishi ni somo la lazima katika Stashahada ya Ualimu linalomwandaa mwalimu kuwa na maarifa, stadi na mwelekeo wa kuwafundisha wanafunzi wote, wakiwemo wenye mahitaji maalumu. Somo hili linazingatia misingi ya ujumuishi, usawa na haki katika elimu, pamoja na matumizi ya mbinu na zana zinazowezesha ujifunzaji kwa kila mwanafunzi.